IQNA

Siku ya Quds

Sayyid Nasrallah atoa wito wa kujitokeza kwa wingi katika Siku ya Kimataifa ya  Quds

18:07 - March 30, 2024
Habari ID: 3478605
IQNA - Katibu Mkuu wa Hizbullah Sayyed Hasan Nasrallah ametoa wito kwa watu kujitokeza kwa wingi barabarani Ijumaa ijayo ambayo inaadhimishwa kama Siku ya Kimataifa ya Quds.

Nasrallah alihutubia siku ya Ijumaa waja katika Dahiyeh ya Beirut na katika usiku wa kwanza wa Laylatul Qadr ambapo aliashiria masuala mbalimbali ya kidini.

Alisisitiza umuhimu wa maombi na kukimbilia uwezo wa Mwenyezi Mungu ili kukabiliana na changamoto za kidunia, ikiwa ni pamoja na makabiliano ya sasa na adui wa Israel huko Lebanon, Gaza na maeneo mengine.

Sayyed Nasrallah alikosoa propaganda za chuki zinazodai kwamba kuomba dua kunaonyesha udhaifu wa Muqawama au harakati za mapambano ya Kiislamu katika medani ya vita, na kuongeza kuwa kusoma dua ni muhimu wakati wa masaibu na furaha vivyo hivyo.

Usaidizi wa Mwenyezi Mungu daima umetusaidia kumshinda adui Muisraeli licha ya kutofautiana kwa uwezo wa kijeshi, Sayyed Nasrallah alisema. Alisema atashughulikia matukio ya hivi karibuni nchini Lebanon Kusini, Gaza na eneo zima hadi Ijumaa ijayo ambayo in Siku ya Kimataifa ya Al-Quds.

"Siku ya Al-Quds mwaka huu inalingana na matukio muhimu."

Sayyid Nasrallah alitoa wito wa ushiriki mkubwa katika mjumuiko wa Hizbullah utakayofanyika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Al-Quds katika Dahiyeh ya Beirut.

Utawala wa Israel umekuwa ukishambulia kwa mabomu Gaza kwa muda wa siku 175 na kuua raia 32,600 wasio na hatia na kujeruhi zaidi ya 75,000 wengine. Hizbullah, kwa upande wake, imeingia katika vita vya mpakani ili kuunga mkono Gaza mbele ya utawala, na kusababisha hasara kubwa kwa vikosi vya uvamizi.

Siku ya Quds au Siku ya kimataifa ya Quds ni Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani. Imam Ruhullah Khomeini muasisi wa Jamhuri ya kiislamu ya Iran tarehe 7 Agosti 1979 alitangaza rasmi Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kila mwaka kuwa, Siku ya Kimataifa ya Quds na siku ya kufanya maandamano kutangaza himaya na uungaji mkono kwa wananchi madhulumu wa Palestina. Katika ujumbe wake wa kuitangaza Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kuwa "Siku ya Kimataifa ya Quds", Imam Khomeini aliwataka Waislamu na wapenda haki kote ulimwenguni kujitokeza kila mwaka katika siku hii kwa ajili ya kutangaza himaya na uungaji mkono wao kwa wananchi wa Palestina na kuungana kwa ajili ya kukata mikono ya utawala haramu wa Israel unaozikalia kwa mabavu ardhi za Palestina huku ukitenda jinai kila uchao dhidi ya wananchi hao madhulumu. Kutangazwa siku ya Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kuwa Siku ya Kimataifa ya Quds kulipokewa kwa mikono miwili na uungaji mkono kutoka kwa wanafikra na shakhsia mbalimbali.

3487748

Habari zinazohusiana
captcha